Tuesday, October 28, 2008

Chozi la mama wa Afrika

baba yuko wapi?
mama kamkumbuka mtoto,kambeba licha ya risasi na sauti za mabomu.
mama analia,analilia nini?huyu huyu mama katuzaa sisi tunaoo mrushia risasi na mabobu,huyu huyu mama katubeba sisi mienzi tisa tumboni lakini shukrani yetu tunamrushia mabomu na risasi.
Afrika tunakwenda wapi?kwanini kila kukicha mapigano yanapamba moto?je hawa waasi wanatoa wapi silaha za moto?jamani umoja wa nchi za Afrika tunafanya nini?kwanini tunasimama na kuangalia tuu?
tumesahau ya Rwanda na Burudi
liberia je!
angola,somalia,
kwanini iwe tu Afrika?
picha kwa hisani ya bbc news,mapigano yanayoendelea huko kwa ndugu zetu congo/zaire.
amani haitafutwi kwa mtutu wa bunduki.

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Amani Kwako Ras. Usemalo ni kweli na unakumbuka waliyosema wenye akili njema juu ya haya? Sikiliza Morgan Heritage katika Anti-War song wakisema "someone knows and some dont care" na ndivyo niaminivyo. Nasio pia alisema kwenye Babylon kuwa "war is not a solution. Never was and never will it be so"
Wapo wengi na kuandika ujumbe wa kila mmoja ni "blog" nyingine. Lakini kupitia vipande vywa kila siku wataelimika tuuu.
Blessings Man