Sunday, October 5, 2008

JE,NI KWELI KUHUSU BLOGU ZETU?

Wakati nikiwa hapa na pale,nilikutana na watu au bin adamu wengi sana, huku mada za kilasiku zikibadilika huku nyingine za kubomoa na nyingine za kujenga sasa ni vema kusikiliza yote then unachuja yale yanayofaa na yasiyofaa.

mada moja mbayo ilinichanga na bado inazidi kunichanganya ni pale mmoja ya wale watu au bin adamu alisimama na kusema UNAWEZ A KUSOMA BLOGU MOJA KISHA UKAJUWA BLOGU ZINGINE ZOTE ZINAZUNGUMZIA NINI(BLOGU ZETU) sikusita kumwambia afafanue.

yule mtu au bin adamu akafafanua hivi,unakuta habari moja blogu zote kwa mfano kama blogu ya rastafarian imeandika kuhusu simba au yanga basi utakuta hii habari katika blogu zingine zote.

Kisha yule mtu au bin adamu akaendelea kuhoji,kulikoni blogu nyingi za Tanzania sio ACTIVE?kulikoni watu au bin adamu wameacha kublogu?

huyu bwana akaendelea kuuliza kulikoni JUMUWATA?

hizi nibaadhi ya changamoto tuanze kuzifanyia kazi.

amani iwe nasi sote.

1 comment:

Christian Bwaya said...

Changamoto ya kweli Rasta.

Kwamba hatuwezi kutofautiana na bado tukazikubali tofauti zetu, hilo ni la kutufikirisha.

Nadhani hatua ya kwanza kuchukua ni kukubali kwamba si lazima tuandikie eneo moja la jamii. Tupanue wigo. Hatuhitaji kublogu siasa ili tuwe wanablogu. Tuonge ladha.

Kuhusu blogu nyingi kutokuwa hai, mimi nadhani hili linaweza kuchangiwa na mwingiliano wa shughuli. Wapo wanablogu kwa mfano, ni wanafunzi ama wanafanya kazi zinazowaweka mbali na mtandao. Inawezekana.

Na wengine, gharama zinaleta mgogoro. Blogu nyingi active zinaendeshwa na watu ambao kwa namna moja ama nyingine wanaishi/kufanya kazi mtandaoni. Ndio maana watu hao wanapobadili makazi ama ofisi, blogu hazibadili posti. Mifano iko wazi.

Hii ni picha halisi ya maisha ya watanzania. Si jambo la ajabu.

Kuhusu JUmuwata mimi sielewi shida ni nini. Nikikumbuka siku wanablogu walipokuwa wakijadili namna ya kuiboresha, mipango mikubwa mikubwa nk nk. Kinachoendelea kinahitaji utafiti.

Asante kwa kuliibua hili Rasta. Nimeandika kwa mcharazo, si unajua muda wa vibanda vya mtandao unavyokimbia?

Amani