baba yuko wapi? mama kamkumbuka mtoto,kambeba licha ya risasi na sauti za mabomu.
mama analia,analilia nini?huyu huyu mama katuzaa sisi tunaoo mrushia risasi na mabobu,huyu huyu mama katubeba sisi mienzi tisa tumboni lakini shukrani yetu tunamrushia mabomu na risasi.
Afrika tunakwenda wapi?kwanini kila kukicha mapigano yanapamba moto?je hawa waasi wanatoa wapi silaha za moto?jamani umoja wa nchi za Afrika tunafanya nini?kwanini tunasimama na kuangalia tuu?
tumesahau ya Rwanda na Burudi
liberia je!
angola,somalia,
kwanini iwe tu Afrika?
picha kwa hisani ya bbc news,mapigano yanayoendelea huko kwa ndugu zetu congo/zaire.
amani haitafutwi kwa mtutu wa bunduki.